Manchester City yaitandika Leicester City kichapo cha mabao 2-0

2892 0

Katika muendelezo wa Ligi Kuu England, timu ya Manchester City ilijipatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Leicester City kwenye uwanja wao. Afueni hii yanakuja baada ya Manchester City kupoteza mechi tano tofauti pasipo kuibuka na ushindi.

Wachezaji Savinho na Erling Haaland walifanikiwa kurudhisha tabasamu kwenye nyuso za mashabiki wa Manchester City kwa kuifungia timu hiyo mabao mawili ambayo yamewachukuwa muda mrefu kupata ushindi katika ligi hiyo.

Katika dakika ya 21, Manchester City kupitia Savinho ilipata bao la kwanza la kuongoza. Bao hili
lilisababishwa na uzembe wa beki wa Leicester City, Jakub Stolarczyk kushindwa kumudu shuti la Phil Foden.

Katika hatua ya kuwahakikishia ushindi Manchester City, katika dakika ya 74, Haaland alifunga bao la pili ambalo lilikuwa ni pasi kutoka kwa Savinho. Bao hili lilikuwa ni la kwanza kwa Haaland baada ya kutokufunga kwenye mashindano 4 tofauti.

Hapo awali, Manchester City ilitoka bila kupata ushindi katika mechi tano mfululizo za mashindano tofauti. Ushindi huu umeifanya Manchester City kufikisha pointi 31 na hivyo kufufua matumaini yake ya kutetea ubingwa wa EPL msimu huu.

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!