Yanga yatembeza kichapo cha mabao 5-0 kwa Fountain Gate

2625 0

Siku ya Jumapili, tarehe 29 Disemba 2024, Yanga ilitembeza kichapo cha mabao 5-0 kwa Fountain Gate
kwenye uwanja wa KCMC Complex.
Kichapo hiki kiligeuka shubiri baada ya uongozi wa timu hiyo kuitimua benchi la ufundi la Fountain Gate
likiongozwa na kocha mkuu Mohamed Muya pamoja na bencho lake kutokana na kutoridhishwa na
matokeo ya juzi.
Baada ya matokeo hayo yakutoridhisha, Uongozi wa Fountain Gate uliamua kuvunja mkataba na kocha
Muya akiwa ni kocha wa 12 kuachana na timu hiyo ya Ligi Kuu.
Dalili za timu ya Fountain Gate kupoteza mechi hiyo zilionekana mapema kutokana na makosa ya mara
kwa mara yaliyosababishwa na safu yake ya ulinzi na kupelekea Yanga kushambulia kwa kasi huku
wakitengeneza nafasi nyingi langoni mwao.
Katika kipindi cha kwanza ndani ya dakika 45, Yanga walipata mabao matatu, la kwanza likifungwa na
kiungo Pacome Zouzoua aliyefunga mara mbili na la tatu kufungwa na Mudathir Yahya.
Kuelekea kipindi cha pili, Yanga ilifanikiwa kuongeza mabao mengine mawali, moja likifungwa na Jackson
Shiga dakika ya 52 na linguine likifungwa na Clement Mzize dakika ya 87 na kupelekea jumla ya mabao
kufikia Matano mpaka dakika ya mwisho.
Ushindi huu wa Yanga umeibakisha timu hii katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu huku ikifikisha pointi 39.

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!