Knock Out ya Mama, yapandisha mabondia watano kuwania mikanda ya ubingwa

3877 0

Usiku wa tarehe 26 Disemba 2024, mashabiki wa ndondi walikusanyika kushuhudia pambano la
mabondia 34 wa ndani na nje ya Tanzania kwenye ukumbi wa Super Dome, Masaki.

Katika Mabondia hao, Kalolo Amir alizichapa na Shile Jelwana wa Afrika Kusini na kuibuka na ushindi wa pointi 100-90 kutoka kwa majaji wawili na kisha jaji mwingine kumpa pointi 99-91 dhidi ya bondia mwenzake. Bondia huyu Mtanzania alitwaa ubingwa wa Pugilistic Syndicate of Tanzania.

Pia katika pambano lingine la raundi 10, Bondia Said Chino alitetea ubingwa wake wa mabara wa
International Boxing Association dhidi ya Michael Klassen wa Afrika Kusini na kuibuka na ushindi wa pointi wa 99-91, 100-90 na 99-91 kutoka kwa majaji watatu.

Bondia Ibrahim Mafia alitwaa ubingwa wa Word Boxing Champion (WBC) Africa dhidi ya Lusizo Manzana wa Afrika Kusini kwa pointi 97-92, 95-94 na 96-93 alizopewa na majaji watatu. Pamoja na ushindi huo, Bondia Ibrahim Mafia alipata jeraha jicho la kushoto raundi ya kwanza.
Katika mapambano mengine mawili ya Knock Out ya Mama, Bondia Salmin alimshinda bondi Adrian Lerassan kutoka Ufilipino na kutwaa ubingwa wa WBF kwa matokeo ya pointi za majaji na pia bondia Yohana Mchanja alitwaa ubingwa wa World Boxing Organisation Globa Championship kwa pinde baaada ya kumshinda bondia Miel Farjado wa Ufilipino kwa pointi 116-112 zilizotolewa na majaji watatu.

Mabondia hawa walioibuka na ushindi wote wataondoka na kitita cha Sh 5 milioni za KO ya Mama ambazo ziliahidiwa kama bonsai kwa bondia yoyote wa Tanzania atakayeshinda ubingwa kwa matokeo ya pointi.

Related Post

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!